Instagram

This is default featured slide 3 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.This theme is Bloggerized by Lasantha Bandara - Premiumbloggertemplates.com.

This is default featured slide 4 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.This theme is Bloggerized by Lasantha Bandara - Premiumbloggertemplates.com.

This is default featured slide 5 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.This theme is Bloggerized by Lasantha Bandara - Premiumbloggertemplates.com.

Saturday, April 13, 2013

TUMIA AVAST FREE ANTIVIRUS KWA ULINZI WA COMPUTER YAKO!

Mimi natumia Avast free Antivirus kwa ulinzi wa computer yangu na inanisaidia sana kuzuia Virus na Vidudu vyote vinavyo hatarisha ulinzi wa computer yangu.
Tafadhari fungua Link hii hapo chini kwa kujipatia Avast Free Antivirus!








http://www.avast.com/get/AZUCA1gS






Bashir aamuru mipaka ya Sudan kufunguliwa

Rais Omar al-Bashir na Salva Kiir
Marais wote wawili wameamua kushirikiana kwa maslahi ya mataifa yao

Rais Omar al-Bashir wa Sudan, katika ziara yake ya kwanza mjini Juba tangu nchi ya Sudan ya Kusini kuwa huru mwaka 2011, ametangaza mipaka kati ya nchi hizo mbili kufunguliwa.
Akizungumza akiwa na rais mwenzake, Salva Kiir, Bw Bashir alitaka pia mataifa hayo mawili kudumisha amani, na kuimarisha uhusiano wa kawaida tena.
Hali ya uhasama iliongezeka kati ya mataifa hayo  mawili mwaka jana, huku kukiwa na wasiwasi wa kuzuka vita.
Uhasama huo umepungua, lakini tofauti kuhusiana na mafuta na ardhi bado upo kati ya nchi hizo mbili.
"Nimewaamuru maafisa wa serikali ya Sudan chama cha maslahi ya raia kushirikiana na ndugu zao katika Jamhuri ya Sudan ya Kusini", Bw Bashir alieleza katika hotuba yake katika mji mkuu wa Sudan ya Kusini, Juba.
"Kamwe hatutarudi katika vita," alieleza.
"Mimi na Bw Kiir tulikubaliana kwamba vita vilifanyika kwa muda mrefu mno."
Kwa upande wake, Bw Kiir alieleza kwamba yeye na Bw Bashir wamekubaliana kwamba watatekeleza masharti yote yaliyoafikiwa ya kuimarisha uhusiano kati ya mataifa yao mawili.

Friday, April 12, 2013

Mzozo kuhusu makampuni ya Mandela

                                                                                                     
                                           


Wanawe rais mstaafu wa Afrika Kusini Nelson Mandela, wameamua kuchukua hatua za kuwaondoa wasaidizi wake watatu kutoka katika makampuni anayoyamiliki.
Hii ni kwa mujibu wa vyombo ya habari nchini humo.
Makaziwe na Zenani Mandela wanadai kuwa watatu hao hawana haki ya kuwa kwenye bodi mbili za kampuni hiyo ambazo ni za thamani ya dola milioni 1.1
Mmoja wa wasaidizi hao, ambaye pia ni wakili wa Mandela, George Bizos,amekana madai hayo.
Kesi hiyo inakuja wakati kuna wasiwasi mkubwa kuhusu afya ya Mandela mwenye umri wa miaka 94
Mandela aliondoka hospitalini baada ya kutibiwa ugonjwa wa mapafu pamoja na homa ya mapafu.
Mandela alilazwa hospitalini mara ya nne katika kipindi cha miaka miwili.
Duru zinasema kuwa kumekuwa na mzozo wa kichinichini tangu mwaka 2005 wa kudhibiti pesa zinazotokana na mauzo kwenye jina la Mandela hususan picha alizokuwa anachora akiwa jela.
Makaziwe na Zenani Mandela waliwasilisha kesi mahakamani wakidai kuwa bwana Bizo, waziri wa nyumba, bwana Tokyo Sexwale na wakili wa zamani wa Mandela, Bally Chuene, hawakuwahi kuteuliwa kama wamiliki au wakurugenzi wa kampuni ya Harmonieux Investment Holdings na Magnifique Investment Holdings, kulingana na gazeti la Star.
Pesa zinazotokana na makampuni hayo zinapaswa kuwafaidi wanawe Mandela na yeye mwenyewe.
"Bizos, Chuene na Sexwale hawakuwahi kuteuliwa rasmi kama washika dau katika kampuni hiyo.''
Bwana Bizos, wakili anayeheshimika sana na ambaye pia ni rafiki wa karibu sana wa bwana Mandela, alisema kuwa watajitetea vikali katika kesi hiyo.
Aliongeza kuwa wanawe Mandela walikuwa wanataka kuuza vitu ambavyo havipaswi kuuzwa .

Boko Haram wakataa msamaha Nigeria





Moja ya mashambulizi ambayo yalifanywa na kundi la Boko Haram mjini Maiduguri

                                  Kundi la wapiganaji wa kiisilamu nchini Nigeria, Boko Haram , limekataa pendekezo la kukubali msamaha.
Wiki jana Rais Goodluck Jonathan, aliuomba mkutano wa maafisa wakuu wa usalama kutafakari swala la kuwapa msamaha wapiganaji hao ili kuwashawishi kusitisha harakati zao.
                                 Tangazo na mtu anayeaminika kuwa kiongozi wa kundi hilo Abubakar Shekau.
Katika miaka ya hivi karibuni, Boko Haram imekuwa ikiendesha kampeini ya ghasia na vurugu katika eneo la Kaskazini mwa nchi, na kuwaua takriban watu 2,000.
Kundi hilo linasema kuwa wapiganaji wake wanapigania kile wanachosema ni taifa la kiisilamu katika eneo la Kaskazini ambalo lina idadi kubwa ya waisilamu.
Bwana Shekau alisema kuwa kundi lake halijakosa hata kidogo, na kwa hivyo msamaha kwao sio jambo la kuzungumzia.
Aidha Shekau aliongeza kuwa ni jeshi la Nigeria ambalo linakiuka haki za waisilamu.
"nashangazwa kwa kuwa serikali ya Nigeria inazungumzia kuhusu msahama. Sisi tumefanya makosa gani? Ni sisi ambao tunapaswa kuwasamehe.'' alinukuliwa akisema Shekau
Mwandishi wa BBC nchini Nigeria,Will Ross, anasema kuwa viongozi wa kisiasa na kidini Kaskazini mwa nchi, wamekuwa wakimtaka rais Jonathan kuwasamehe wapiganaji hao, wakisema kuwa hatua za kijeshi dhidi ya wapiganaji hao hazisaidii kuleta amani.
Jopo la kutoa msahama liliundwa na serikali wiki jana na linajumuisha waakilishi wa jeshi.

Thursday, April 4, 2013

Zawadi ya dola milioni 5 kumkamata Kony


Marekani imeahidi zawadi ya dola milioni tano kwa yeyote atakayetoa maelezo yatakayosaidia kukamatwa kwa kiongozi wa waasi wa Lords resistance Army nchini Uganda Joseph Kony.
Bwana Kony anadaiwa kuongoza maasi ya zaidi ya miongo miwili nchini Uganda na anatakiwa na mahakama ya kimataifa ya Uhalifu ICC kwa mTangazo hili limekuja huku jeshi la Uganda likiakhirisha msako wa kiongoiz huyo wa waasi, katika jamuhuri ya Afrika ya kati, baada ya kusema kuwa wanatatizwa na serikali mpya ya mpito.

Kony na wapiganaji wake wako katika maficho yanayopakana na nchi jirani za Jamuhuri ya Afrika ya Kati, ikiwemo Sudan, Jamuhuri ya kidemokrais ya Congo na Uganda.
Maafisa wa Marekani wanasema kuwa zawadi hiyo pia inatolewa kwa yeyote atakayetoa taarifa kuwahusu viongozi wengine wa waasi wa LRA Okot Odhiambo na Dominic Ongwen.
Kundi la LRA limewatesa watu na kuwadhalilisha watoto nchini Uganda, na kote katika eneo hilo. Waziri wa mambo ya kigeni wa Marekani John Kerry alinukuliwa akisema kwenye jarida la Huffington Post siku ya Jumatano.
Bwana Kerry alisema kuwa Kony na viongozi wengine wa LRA , hawatapatikana kwa urahisi.
Kundi la LRA limetawanyika kwa makundi na waasi, walioko katika sehemu kubwa ya nchi kwenye maficho ambayo kwa kweli ni vigumu kuyapata, wakitawala eneo hilo kwa kutumia vitisho na kuwatia watu hofu.
Mapema, jeshi la Uganda katika Jamuhuri ya Afrika ya Kati, lilisitisha msako wao wa Kony na kurejea katika kambi zao za kijeshi.ashtaka ya uhalifu wa kivita.

Tisho la Korea Kaskazini kwa Marekani

Marekani imepeleka mitambo ya kukinga makombora katika kisiwa cha Guam katika bahari ya Pacific huku Korea Kaskazini ikitishia kurusha makombora ya nuklia nchini humo.


Idara ya ulinzi ya nchi hiyo imesema kuwa mitambo hiyo itakuwa tayari katika kipindi cha wiki kadhaa , na kuongeza kwa zana za kivita ambazo zilipelekwa katika eneo hilo.Korea Kaskazini ilitaja kisiwa cha Guam kuwa miongoni mwa maeneo yanayolengwa kwa mashambulizi ikiwemo Hawaii na Marekani.
Korea Kaskazini haidhaniwi kuwa na teknolojia ya kutosha kushambulia Marekani kwa zana za nuklia au makombora ya masafa marefu.
Korea Kaskazini inasema kwamba imewaweka wanajeshi wake, tayari kwa shambulio dhidi ya Marekani ikiwemo kutumia zana za nyukilia.
Taarifa hii imejiri wakati Marekani imeimarisha mitambo yake ya kukinga makombora katika kisiwa cha Guam kilichoko bahari ya Pacific.
Idara ya ulinzi ya Korea Kaskazini imesema inatoa taarifa kwa Marekani kwamba jeshi lipo tayari kushambulia bila huruma, kile imetaja kama vitisho vya Marekani dhidi yake.
Utawala wa Pyongyang ulionekana kukerwa na hatua ya Marekani ya hivi maajuzi ambapo wanajeshi wake walifanya mafunzo ya pamoja na ambayo yalihusisha utumizi wa zana za kivita.
Hata hivyo wachanganuzi wamesema Korea Kaskazini haina silaha ambazo zinaweza kushambulia ardhi ya Marekani, japo katika siku za karibuni imefanya majaribio ya makombora ua masafa marefu.
Hapo jana Jumatano, Korea Kaskazini iliwazuia wafanyikazi wa Korea Kusini kuvuka mpaka kuelekea katika viwanda vya pamoja vinavyomilikiwa na nchi mbili, na hivyo kukatiza uhusiano uliobaki kati yake na Kusini.
Baadhi wanaona malumbano ya sasa kama hatua ya Korea Kaskazini kushinikiza Marekani kuanzisha mazungumzo ya pamoja ambayo yataafikia mkataba wa amani.

Tutu ashinda tuzo ya dola milioni 1.6

Askofu wa zamani wa kanisa la Anglikana Afrika Kusini katika jimbo la Cape Town Desmond Tutu, ametajwa mshindi wa tuzo ya mwaka huu ya Templeton ambapo atapokea kima cha Dola milioni 1.6

Tutu mwenye miaka 87 ametaja Tuzo hii kama ushindi kwa wote wanaotetea haki za wanyonge bila kubagua.Askofu Tutu atapokea tuzo hiyo mwezi ujao mjini London, Uingereza.
Akijibu ushindi huo mwanaharakati huyo wa haki za binadamu amesema kwamba jamii huwatuza wote wanaotetea haki yao.
Tuzo hii ilianzishwa mwaka wa 1972 kutolewa kwa raia ambao huchangia zaidi masuala ya imani na dini bila ubaguzi, ambaye pia hutetea haki za wanyonge.
Mwasisi wa tuzo hii Sir John Templeton alikua raia wa Marekani lakini akahamia Uingereza ambapo pia alituzwa na Malkia kwa mchango wake kwa jamii mwaka 1987.
Alifariki dunia mwaka 2008.Mwaka jana Tuzo ya Templeton ilitolewa kwa Kiongozi wa Kiroho wa Tibet Dalai Lama.
Mwaka jana Askofu Tutu alipokea dola Milioni moja kutoka kwa Wakfu wa Mo' Ibrahim ambayo hutoa tuzo kwa raia waafrika ambao hutetea haki na ukweli na kutetea utawala bora.
Desmond Tutu alishinda tuzo ya amani ya Nobel mwaka 1984 kutokana na harakati zake dhidi ya ubaguzi wa rangi nchini Afrika Kusini.

Wednesday, April 3, 2013

Bozize adai Chad ilichangia kumpindua

Rais aliyeng'olewa mamlakani katika Jamuhuri ya Afrika ya Kati, ametuhumu serikali ya Chad kwa kuwasaidia waasi waliompindua mwezi jana.
Francois Bozize, aliambia BBC, kuwa wanajeshi maalum wa Chad waliongoza operesheni ya mwisho ya waasi mwezi jana pamoja na kuwaua wanajeshi wa Afrika Kusini.Chad, ambayo ni mwenyeji wa mkutano wa dharura wa kikanda kuhusu Afrika ya kati, haijajibu tuhuma hizo.
Bwana Bozize alisema kuwa aliomba kushirikishwa kwenye mkutano huo lakini akakataliwa.
Lakini rais wa Afrika Kusini, Jacob Zuma ni mmoja wa marais wanaohudhuria mkutano huo wa nchi za Magharibi.
Wanajeshi kumi na watatu wa Afrika Kusini waliuawa kwenye makabiliano mjini Bangui, wakati waasi wa kundi la Seleka, walipotwaa mamlaka baada ya mkataba wa amani uliokuwa umependekezwa na rais Bozize kutupiliwa mbali.
Tukio hilo limesababisha taharuki nchini Afrika Kusini. Chama tawala ANC, kimekanusha madai kuwa wanajeshi walikuwepo nchini humo kwa sababu ya maslahi yake ya uchimbaji madini.
Serikali ya Afrika Kusini inasema kuwa wanajeshi wake walikuwa wanatoa mafunzo kwa majeshi ya serikali.
Wiki jana bwana Zuma, alisema kuwa wanajeshi wa Afrika Kusini, walifariki katika makabiliano makali yaliyochukua masaa tisa kupambana na waasi.
Bwana Bozize, alitwaa mamlaka katika mapinduzi mwaka 2003 na kushinda uchaguzi mara mbili anasema ameshangazwa na hatua ya Chad.

Rais mstaafu Mandela aendelea kupata nafuu



Rais mstaafu wa Afrika Kusini Nelson Mandela anaendelea kupata nafuu wakati akitibiwa homa ya mapafu, kwa mujibu wa madaktari wake.
Taarifa kutoka kwa ofisi ya rais Jacob Zuma, ilisema kuwa Mandela alitembelewa na jamaa zake wakati akiendelea kupokea matibabu.Inaarifiwa kwa sasa hali yake inaendelea kuwa nzuri ikilinganishwa na alivyokuwa wakati alipolazwa hospitalini tarehe 27 mwezi Machi Mandela amelazwa hospitalini sasa kwa mara ya nne katika kipindi cha miaka miwili.
Mnamo Disemba alitibiwa homa ya mapafu na kibofu na alikaa hospitalini sana kuliko wakatii mwingine wowote.
Mnamo Februari alitibiwa maradhi ya tumbo.
Wiki jana rais huyo wa zamani mwenye umri wa miaka 94,pia alibitiwa maradhi ya mapafu.
Mpaka sasa hakuna taarifa zozote kuhusu muda atakaosalia kuwa hospitalini.
Bwana Mandela alikuwa rais wa Afrika Kusini tangu mwaka 1994 hadi 1999 na anatazamiwa na wengi kama baba wa taifa hilo kwa kupigana dhidi ya enzi ya utawala wa ubaguzi wa rangi.
Licha ya kufungwa kwa miaka mingi jela, Mandela alisema aliwasamehe maadui zake na kuwataka wananchi wa taifa hilo kushirikiana.
Alishinda tuzo ya amani ya Nobel mwaka 1993

Msako wa Kony wasitishwa Afrika ya Kati

Serikali ya Uganda inasema kuwa imesitisha msako wake wa kiongozi mtoro wa waasi wa LRA Joseph Kony, katika Jamuhuri ya Afrika ya Kati.
Uganda inasema imeamua kuchukua hatua hiyo kufuatia mgogoro wa kisiasa unaokumba taifa hilo baada ya rais Francois Bozize kung'olewa mamlakani.

Pia imeelezea kuwa serikali ya mpito inayoongozwa na kiongozi wa waasi imetatiza shughuli zao.
Uganda inasema kuwa wanajeshi wake katika eneo hilo ambako waasi walichukua mamlaka siku kumi zilizopita, watasalia katika kambi zao hadi muungano wa Afrika utakapotoa mwongozo.
Joseph Kony anayeongoza kundi la waasi wa LRA, anatakikana na mahakama ya kimataifa ya jinai kwa tuhuma za uhalifu wa kivita.
Anaaminika kujificha na wapiganaji wake katika misitu inayopakana na Jamuhuri ya Afrika ya Kati, Sudan Kusini na Jamuhuri ya kidemokrasia ya Congo.

Mgororo wa Korea mbili watokota

Korea ya kusini imesema kuwa nchi jirani ya Korea Kaskazini inawazuia raia wake kwenda kazini upande wa pili wa mpaka katika kiwanda.
Wizara inayohusika na kuleta utangamano kati ya nchi hizo mbili mjini Seoul, imetoa wito kwa serikali ya Pyong Yang itawaruhusu raia hao wa Korea Kusini kurejelea kazi katika kiwanda cha Korean Kusini .


Meneja wengi wa kiwanda hicho wamesusia kwenda kazini wakihofia kuwa watazuiwa kuingia.
Awali Marekani ilitoa onyo kwa Korea Kaskazini dhidi ya kufungua upya kinu cha kutengenezea silaha za nuclear.
Waziri wa nchi za kigeni wa Marekani John Kerry amesema kuwa iwapo Korea Kaskazini itaendelea na mipango yake iliyotangaza hapo jana ya Nuclear, basi utakuwa uchokozi wenye madhara makubwa.
Marekani imeshutumu Korea ya Kaskazini kuhatarisha maisha ya watu bila kujali.
Hapo awali vitisho kutoka kwa Korea Kaskazini, vimekuwa vikipuuzwa tu kama vitisho vya kawaida lakini sasa Marekani imeanza kuwa na wasiwasi kuhusiana na kiongozi chipukizi wa Korea Kaskazini Kim Jong Un , kuwa huenda vitisho vyake sio vya bure.
Akiongea na mwenzake wa Korea Kusini, waziri wa mashauri ya kigeni, wa Marekani , John Kery alitaja kuwa vitosho vya hivi maajuzi ni vya ukweli fulani , na hatari bila kujali lolote.
Alisema kuna muda wa kutosha kwa Korea Kasakazini kubadili mwenendo wake ili kutilia mkazo zaidi mahitaji ya watu wa eneo hlo ambayo Kerry alisema Marekani iko tayari kusaidia.
Lakini ushawishi wa kurejesha misaada huenda usibadilishe msimamo wa Korea Kaskazini. Marekani imetaka Uchina ishauriane na jirani wake wa Korea Kaskazini . Kwa wakati huu Marekani inaendelea kunyosha misuli yake ya kijeshi .
Makao makuu ya Jeshi la Marekani , Pentagon yalithibitisha yatatuma zana nyingine za kuharibu makombora katika eneo hilo.