Mashada na Picha ya Rais mstaafu wa Afrika Kusini Marehemu Nelson
Mandela anayetarajiwa kuzikwa jumapili ya tarehe 15 Disemba, 2013
Johannesburg. Viongozi zaidi ya sabini wakiwamo wakuu wa nchi na
Serikali wanatarajiwa kushiriki hatua mbalimbali za safari ya mwisho ya
Mzee Mandela aliyefariki Alhamisi ya Desemba tano usiku.
Anatarajiwa kuzikwa Jumapili ijayo, Desemba 15,
2013 katika Kijiji cha Qunu alikokulia, mazishi ambayo yanatarajiwa
kuwavuta maelfu ya watu kutoka kona mbalimbali za dunia.
Hata hivyo hadi jana maofisa wa Serikali ya Afrika
Kusini walisema walikuwa bado hawajapata orodha kamili ya viongozi wote
watakaohudhuria, l pia wakashindwa kusema iwapo Rais Obama atakwenda
Qunu au atashiriki katika hatua nyingine za awali za msiba huo kabla ya
mazishi ya Jumapili.
Msemaji wa Ikulu ya Marekani, Jay Carney
alinukuliwa akithibitisha kwamba Obama na mkewe Michele watashiriki
katika msiba huo lakini hakuwa tayari kueleza suala hilo kwa undani.
Habari zaidi zilizopatikana jana mjini Johanesburg zinasema Rais wa
Brazil, Dilma Rousseff atakuwa miongoni mwa wageni mashuhuri
watakaoshiriki.
Balozi wa Marekani nchini Afrika Kusini, anasema
kuwa: “Rais Obama, amethibitisha kushiriki mazishi ya Madiba” (akirejea)
jina maarufu la Mzee Mandela, taarifa ambayo ilitiliwa na nguvu na
habari zilizoinukuu Ikulu ya Washington ikithibitisha ujio wa kiongozi
huyo pamoja na watanguliza wake; George W. Bush na Bill Clinton.
Vyombo mbalimbali vya habari vilinukuu taarifa ya
Ikulu ya Marekani ikisema: “Rais Obama na mkewe watakwenda Afrika Kusini
wiki ijayo kwa ajili ya kutoa heshima za mwisho kwa ajili ya kumbukumbu
ya Nelson Mandela na watashiriki katika tukio hilo la kukumbukwa.”
Rais wa Afrika Kusini, Jacob Zuma alitangaza
ratiba ya maombolezo ya shujaa huyo aliyeongoza vita dhidi ya sera za
ubaguzi wa rangi zilizokuwa zikitekelezwa na Makaburu na jana ilikuwa ni
siku ya maombi ya kitaifa kwa ajili ya Mzee Mandela.
Leo Jumanne kutakuwa na tukio la kitaifa katika
Uwanja wa Michezo wa FNB, Johannesburg ambako ni sehemu ya hitimisho ya
safari ya Mandela huku watu zaidi ya 80,000 wakitarajiwa kuhudhuria na
kati ya kesho Jumatano na Ijumaa, mwili wa Mandela utakuwa katika
Majengo la Umoja (Union Buildings) Pretoria ambako utaangwa kwa siku
tatu mfululizo.
Mkurugenzi wa Habari na Mawasiliano wa Afrika
KusiniNeo Momodu aliwaambia waandishi wa habari jijini Johannesburg kuwa
watuwa Pretoria watakuwa na nafasi ya kushuhudia mwili wa Mandela
ukisafirishwa kutoka chumba cha kuhifadhia maiti kwenda Jengo la Umoja
kila asubuhi kwa siku tatu mfululizo.
Momudu anasema mitaa ambayo mwili huo utakuwa
ukipitishwa itatangazwa ili kuwezesha wakazi wake na wananchi wengine
kupata fursa ya kujipanga pembezoni mwake kwa ajili ya kutoa heshima za
mwisho kwa kiongozi huyo.
“Njia ambazo mwili wa marehemu utakuwa ukipitishwa
kila asubuhi kutoka chumba cha kuhifadhia kwa ajili ya kupelekwa kupewa
heshima za mwisho, zitatangazwa na tutawaomba wananchi kujipanga
pembezoni mwa njia hizo wakati mwili huo ukipita katika mitaa hiyo ya
Pretoria,” anasema.
Hata hivyo, Momodu anasema utaratibu wa kutoa
heshima za mwisho utaratibiwa na kuna uwezekano mkubwa kwamba si kila
mtu atakayeweza kuingia katika eneo hilo na kwamba kila mmoja
atakayeingia lazima awe na kitambulisho maalumu.
Anasema kutakuwa na eneo maalumu la kusubiri kuingia kwa ajili ya kutoa heshima za mwisho na kwamba watakafanikiwa kupata ruhusa ya kwenda kuaga, watakuwa wakipakiwa kwenye mabasi maalumu yaliyoandaliwa kwa ajili ya kazi hiyo na watarejeshwa na mabasi hayo.
Anasema kutakuwa na eneo maalumu la kusubiri kuingia kwa ajili ya kutoa heshima za mwisho na kwamba watakafanikiwa kupata ruhusa ya kwenda kuaga, watakuwa wakipakiwa kwenye mabasi maalumu yaliyoandaliwa kwa ajili ya kazi hiyo na watarejeshwa na mabasi hayo.
Jumamosi, Desemba 14, mwili wa Mandela utasafirishwa kwenda Qunu ambako Jumapili Desemba 15, utazikwa rasmi.
0 comments:
Post a Comment