MADRID, HISPANIA
INGAWA wanacheza pamoja katika timu ya taifa ya
Brazil, lakini beki wa kushoto wa Real Madrid, Marcelo amempania vilivyo
staa mpya wa Barcelona, Neymar, wakikutana katika mechi ya El Classico.
Mechi hiyo imekuwa ikizua ukorofi mwingi ndani ya
uwanja katika miaka ya karibuni, huku wachezaji wanaotoka katika taifa
moja wakiweza kutiana ngumi mkononi. Marcelo anaamini Neymar atakiona
cha moto.
“Ni jambo la kawaida. Tayari tumeshaonyeshana kazi
na Dani Alves. Baada ya mechi tunarudi kuwa kitu kimoja tena. Itakuwa
hivyo hivyo kwa Neymar. Ni rafiki yangu mkubwa, lakini hiyo haitakuwa
hivyo katika mechi dhidi ya Real Madrid,” alisema Marcelo.
Marcelo alikataa kuongea lolote kuhusu uhamisho
uliokwama wa staa wa Tottenham, Gareth Bale kwa madai kwamba anapenda
kuwazungumzia zaidi wachezaji waliopo.
0 comments:
Post a Comment