b
Bondia Francis Cheka (kushoto) na Phil Williams kutoka Marekani, kwa pamoja wakiwa wameshika Taji la Ndondi la Dunia (WBF) mara baada ya kumaliza kupima uzito katika Ukumbi wa Idara Habari Maelezo jana, tayari kuzikunja leo kwenye Ukumbi wa Diamond Jubilee, Dar es Salaam. Picha na Michael Matemanga.
Dar es Salaam. Bingwa wa Masumbwi, Francis Cheka amesema dhamira ya kumtandika mpinzani wake, Phil Williams kutoka Marekani katika pambano lao usiku wa leo, iko palepale.
“Siwezi kumwangusha Rais Jakaya Kikwete, namwahidi nitashinda mchezo wa leo na kuubakisha mkanda wa ubingwa Tanzania,” alisema Cheka wakati akiongea na Mwananchi jana.
Cheka anashuka ulingoni, Diamond Jubilee kuzikunja na Williams katika pambano la kuwania Ubingwa wa Dunia (WBF), huku Makamu wa Rais, Gharib Bilal akiwa mgeni rasmi kumwakilisha Kikwete.
Mabondia hao, jana walipima uzito jijini Dar es Salaam tayari kwa pambano hilo linalosubiriwa kwa hamu kubwa na mashabiki wa ndondi nchini.
“Najua JK (Jakaya Kikwete) ni mpenda michezo na anatoa sapoti kwenye michezo, hivyo namwahidi kufanya kweli leo,” alisema Cheka na kuongeza: “Nimejipanga kushinda pambano hili, nilishasema tangu awali, narudia kusema tena, sitawaangusha mashabiki wangu.”
Aliongeza: “Niko tayari kufia uwanjani, lakini siyo kuliona taji linaondoka Tanzania. Nitamaliza kazi kwa mafanikio.
Kwa upande wake, Williams alisema amekuja kushindana na siyo kinyume chake, hivyo anajiandaa kutoa upinzan mkali dhidi ya mpinzani wake.
Mwanamasumbwi huyo anashuka dimbani ikiwa ni wiki mbili kupita tangu amshinde kwa pointi bondia wa Malawi, Chiotcha Chimwemwe. Pia kutakuwa na mapambano ya utangulizi kati ya Thomas Mashali na Mada Maugo watakaowania Ubingwa wa WBF Afrika.
0 comments:
Post a Comment