Waziri wa Uchukuzi, Dk Harrison Mwakyembe
Dar es Salaam. Waziri wa Uchukuzi, Dk Harrison Mwakyembe
amewashukia waendesha mashitaka na wapelelezi kesi zinazohusiana na dawa
za kulevya kuwa hadi sasa zimefikia 36 lakini hakuna taarifa zake.
Mwakyembe aliyasema hayo wakati akizungumza kwenye
Kipindi cha Jenerali On Monday kilichorushwa na Kituo cha Televisheni
cha Channel Ten juzi usiku.
Mwananchi iliwasiliana na Mkurugenzi wa Mashtaka,
Elieza Feleshi kuhusiana na hilo, lakini hata hivyo simu yake ilikuwa
haipatikani. Hata ilipofika ofisini kwake, ilielezwa kuwa alikuwa kwenye
mkutano.
Kamanda wa Kikosi cha Kuzuia Dawa za Kulevya,
Godfrey Nzowa alipotafutwa jana kuzungumzia hali hiyo, simu yake ilikuwa
haipatikani.
“Kila anayekamatwa lazima achukuliwe hatua stahiki
kwa kosa lake na hakuna sababu ya kuleana wala kuogopana,” alisema Dk
Mwakyembe ambaye ametangaza kujitoa muhanga kupambana na mtandao wa dawa
za kulevya nchini.
Mwakyembe aliyekuwa akizungumzia mapambano hayo
aliyoyaanzisha ya dawa za kulevya, alirejea sakata la kuvushwa dawa za
kulevya Uwanja wa Ndege wa Julius Nyerere, JNIA alisema: “Wote
tumewafukuza kazi kwa sababu walihusika kupitisha dawa hizo.”
Hata hivyo, Mkurungenzi wa JNIA, Moses Malaki
akizungumza na gazeti hili, alisema juzi kuwa utaratibu wa kuwapatia
barua zao umekamilika na sasa kinachofuata ni utaratibu wa kuunda tume
ambao utafanyika wakati wowote kwa ajili ya uchunguzi na kuwahoji.
Wafanyakazi hao wa JNIA, wanatuhumiwa kula njama za kupitisha kilo 150 za dawa za kulevya aina ya Crystal Methamphetamine.
Dk Mwakyembe alisema pia kuwa watu hao watafukuzwa
kazi pamoja na wahusika wengine. “Ule mkanda unaonyesha watu
walivyokuwa wakihangaika siku ile pale. Kuna askari anaonekana anasaidia
kupitisha mizigo kwenye mashine, huyu askari ni kazi yake hii?
“Wapo watu walikuwa wakihangaika huku na huko,
yaani walikuwa hawatulii, ni kama sinema, wengine wako ‘bize’ na simu
badala ya kufanya ukaguzi, sasa tumewafukuza...Najua wapo wengine,
nasema kama mtu aliona, alisikia na hakusema naye atakwenda na maji.
Alisema amewasiliana na Waziri wa Mambo ya Ndani,
Dk Emmanuel Nchimbi kwa ajili ya kufanikisha kazi hiyo. “Nimemwomba
Waziri wa Mambo ya Ndani tufanye kazi na lazima tuumalize huu mtandao.”
Akizungumzia ukaguzi wa mizigo, Dk Mwakyembe
alisema lazima mizigo yote ikaguliwe hata bandarini. “Pale Uwanja wa
Ndege kuna mitambo pengine bora zaidi kuliko mahala pengine popote
Afrika na kama haitoshi, tuongeze mingine zaidi.
Alipoulizwa kama atakuwa na ubavu wa kuzuia ‘unga’ wa vigogo, Mwakyembe alisema: “Kigogo yeyote atakayejitokeza nitamkamata tu...Ajitokeze sasa hivi aone. Nimeshangazwa na kilo 180 kupita, huu mtandao wa kipuuzi lazima kuuvunja.
Alipoulizwa kama atakuwa na ubavu wa kuzuia ‘unga’ wa vigogo, Mwakyembe alisema: “Kigogo yeyote atakayejitokeza nitamkamata tu...Ajitokeze sasa hivi aone. Nimeshangazwa na kilo 180 kupita, huu mtandao wa kipuuzi lazima kuuvunja.
“Asije mtu akatarajia kuchekewa, ataondoka.
Atakayeruhusu mtu kupita na dawa za kulevya, tukibaini, ataondoka tu.
Wako wengi wanatafuta kazi. Tulijiachia vya kutosha, na sasa basi.”
Akizungumzia hali ilivyo Bandarini kwa sasa,
alisema wameimarisha udhibiti wa upotevu wa makontena. “Hali kwa sasa ni
nzuri, ilikuwa aibu, kila siku makontena yanapotea, tulianzisha
utaratibu, kontena likipotea kitengo kizima wanakatwa mishahara
kulipia,” alisema.
Alisema pia kumeanzishwa utaratibu wa kukagua mizigo yote inayoingia na kutoka.
0 comments:
Post a Comment